MARLLEN

NCHI ALIYOTOKEA: MOZAMBIQUE
AINA YA MUZIKI: RNB

 

KURASA ZA KIJAMII

 

Marllen alirekodi single yake ya kwanza “Xinate” uliotengenezwa na N’sta akiwa na umri wa miaka 18 baada ya kushiriki shoo ya “Fantastico” inayoandaa maonyesho ya ku-dance akiwa na kundi lake lililokuwa linaitwa “Kina Fusion” ambalo limempatia umaarufu mkubwa.  Aliachia albamu yake ya kwanza inayoitwa, ‘Negra Africana’, iliyompatia chance za kualikwa na kufanya maonyesho katika nchi mbalimbali Kusini mwa Afrika.

Mwaka 2008, alitoa albamu yake ya pili “Preta Negra” iliyosababisha ulimwengu wake wa muziki kuanza kung’aa.  Kibao chake cha kwanza kutoka kwenye albamu ya “Preta Negra” iliyoorekodiwa mwaka 2007 kilirekodi mafanikio makubwa kiasi kwamba yeye akaanza kutambulika kwa jina “Preta Negra” au “Marllen Petra Negra” na kumwongezea umaarufu barani Afrika.

Marllen aliwahi kufanya onyesho pamoja na mwimbaji wa Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka anayejulikana pia kama “Malkia wa Afrika” kwenye kilele cha African Union Summit, zilizofanyika Kampala Uganda mwaka 2010.  Mwaka 2012 alimaliza elimu yake ya Usimamizi wa Utamaduni, iliyomwongezea ujuzi maradufu wa tasnia ya sanaa.

Mwaka 2013, baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza, Marllen alirekodi na kuuza single yake maarufu “Muxtado”, maana yake ni Ndoa.  Kwa sasa Merlien yupo kwenye mchakato wa kukamilisha albamu yake ya tatu inayobeba jina la “Muxtado” ambayo ameiandaa kwa ajili ya kuelezea kipindi cha kuanza maisha ya muziki hadi kuolewa.  Muziki  ni kitu muhimu sana kwa Marllen kwa sababu unaelezea jinsi alivyoanza kazi ya muziki akiwa na miaka 15 wakati akiwa mwigizaji.  Kuingia kwake kwenye muziki alichukua yale yote aliyojifunza kwenye majukwaa kuanzia kwenye uimbaji, uchezaji na kucharaza gitaa. Wakati wa mapumziko, mara kwa mara hupendelea kusikiliza miziki yake huku akijiburudisha na maji na matunda.