LILIAN MBABAZI

NCHI ALIYOTOKEA: UGANDA
AINA YA MUZIKI: RNB

 

KURASA ZA KIJAMII

    

Baada ya kujiondoa kutoka kwenye kundi la wasichana wa Kiganda Blu*3  alichanua miongoni mwa waimbaji wa juu kabisa wanawake nchini Uganda, akitumia  mtindo wake  tofauti wa muziki ambao unasemekana kuwa una mahadhi ya kati ya RnB/Soul  ukipambwa kwa ladha za Kiafrika na Kimagharibi.

Mapenzi yake makubwa ya kumiliki jukwaa anapofanya live show yanamfanya ang’ae kila anapopanda jukwaani, kwa jinsi anavyowapagawisha mashabiki wake kwa sauti yake yenye nguvu na mvuto.  Akiwa katika bendi yake ya Sundowners, Lillian huimba nyimbo zilizoiimbwa na wasanii maarufu kama vile Alicia, Key’s, India Arice na Lauryn Hill ikiwa ni pamoja na zile zilizotungwa na bendi yake. 
Lillian ana orodha ya nyimbo ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa, Afrika Mashariki na kwa sasa yuko katika maandalizi ya albamu yake.  Amefanya Collabo nyingi naa baadhi ya wasanii wa maarufu Afrika Mashariki kama vile Navio, Radio & Weasel, Ay, P-Unit, Kitoko, The Mith, Keko, Cindy, Ekky & DJ Global.

Lillian alishiriki kwenye onyesho la sherehe za Umoja Festival nchini Msumbiji (mwaka 2011 na 2013) akiwa na mwanamuziki nguli wa Afrika Oliver Mtukuzi, mbele ya umati mkubwa wa watazamaji 30,000 na kwenye onyesho kubwa la sherehe za maadhimisho ya miaka hamsini (50) ya uhuru wa Uganda tarehe (8 Oktoba, 2012). 
Lillian akiwa na kundi la Sundowners walifanya onyesho kwenye sherehe za Ubalozi wa Uganda Kigali nchini Rwanda, mbele ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paulo Kagame.

Vilevile, Lillian alishiriki kwenye onyesho katika sherehe za Coke Studio Afrika 2013, akiimba wimbo wake ulioboreshwa  kwa mwendo wa kasi wa wimbo wake wa “Danger” (Barua ya mapenzi) muziki mchanganyiko wa Maria Salome, wa Temi Dollface (Nigeria) na wimbo wa taarabu ‘Bahati’ aliouimba pamoja na kundi taarabu la Culture Musical Club (Zanzibar).