JOSE VALDEMIRO

NCHI ALIYOTOKEA: MOZAMBIQUE
AINA YA MUZIKI: RNB

 

KURASA ZA KIJAMII

 

José mwenye miaka 30 a.k.a VJ, alirekodi albamu yake ya kwanza inayoitwa “My Style” akisaidiwa na watayarishaji mbalimbali wa muziki nchini Msumbiji mnamo mwaka 2006, iliyomweka kwenye soko kuu la muziki nchini humo. Mwaka 2007, alifanya onyesho lake la kwanza la Kimataifa nchini Afika Kusini na Swaziland. Mwaka  2008, alitoa albamu yake ya pili iliyoitwa “Recomecar” ambapo iliyosheheni miondoko ya  Afro na Zouk. Albamu hii ilipata mafaniko na ilimpatia ushindi wa tuzo nne za juu nchini humo. José amekuwa akifanya utafiti wa midundo ya kienyeji, akichanganya na baadhi ya nyimbo maarufu za kikabila kwa kuingiza mahadhi hayo mapya; hii imeonekana kwenye albamu yake ya tatu aliyoitoa mwaka 2013 inayojulikana kwa jina la ”Minha Historia” iliyompelekea José kuungana na Zena Bacar na vilevile wimbo wake kutoka kwa Malada, ambazo zote mbili zilivuma sana nchini Msumbiji katika miaka ya 80,baada ya kipindi cha miaka kumi akiwa katika kazi yake ya muziki , pasipo ubishi, José amekuwa gumzo na maarufu kuliko wote Msumbiji, akiwa ameshiriki jukwaani na wanamuziki kutoka PALOP (Nchi za Kiafrika  Zinazozungumza Kireno) kama vile Paulo Flores, Matias Damasio, Don Kikas, na Stewart Sukuma na nyinginezo.