JOH MAKINI

NCHI ALIYOTOKEA: TANZANIA
AINA YA MUZIK: HIP-HOP

 

KURASA ZA KIJAMII

  

Joh Makini ni mtanzania mwanamuziki wa “kufoka” na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Weusi Company (Kampuni ya Kurekodi); ni msanii maarufu na kioo cha heshima katika muziki wa Hip-Hop, mtunzi na mtengenezaji Tanzania.  Joh Makin ana sifa ya kipekee katika matumizi ya sitiari na ubunifu wa kutupia free style na uwezo wa kucheza na ngeli.  Joh Makin ana mvuto wa kipekee kwenye jukwaa unaowakuna masabiki wa muziki kutokana na uzoefu wake katika ushereheshaji.  Mtanzania huyu maarufu amewahi kupanda jukwaani na wanamuziki maarufu wa Afrika Mashariki kama vile Nonini, Chamileon, Psquare, Dbanj, Diomond Juliana Wyre na Prezzo.  Vilevile amefanya maonyesho na wasanii wa kimataifa kama vile Jay-z, Ja Rule, 50 Cent, Fat Joe, Eve, Busta Rhymes, Sean Kingston, Fabulous na Kat Deluna.  Nyimbo zake za “Karibu Tena”, Stimu Zimelipiwa”, “Bei ya Makaa, “Nje ya Box” na Gere” Zimekuwa zikipigwa katika vituo vyote vya redio na Televisheni hapa Afrika Mashariki.

Joh Makin alianza kufanya shughuli za muziki kama hobby, akatoa rekodi yake ya kwanza mwaka 2002 ijngawa haikuvuma.  Aliendelea na muziki hadi mwaka 2006, ambapo alianza kufanya muziki kama kazi yake.  Yeye ni mtunzi wa sehemu kubwa ya nyimbo zake ingawa kwa nyakati kadhaa hupata ushauri kutoka kwenye kundi lake la Weusi.  Maisha yake, mazingira yake, na ari yake ni kuwajengea uelewa na kuelimisha wengine, ndivyo vitu vinavyomsukuma Joh Makin kuandika mashairi yake yanayofuata utashi huo.  Mwanzoni jina lake kwenye jukwaa alijulikana kama “Rapture” lakini baada ya kukua kimuziki na kuchagua mtindo wa muziki anaoutaka, alibadilisha jina na kurudi kwenye jina la “Joh Makin”.  Muziki wake umebadilika kwa miaka kadhaa akijaribu kuendana na wakati.