JAY A

NCHI ALIYOTOKEA: KENYA
AINA YA MUZIKI: HIP-HOP, RNB

 

KURASA ZA KIJAMII

   

Jay A  mwenye umri wa miaka 23, aliingia kwenye tasnia ya muziki miaka miwili na nusu iliyopita na ndani ya  kipindi cha chini ya miezi sita tu alifanikiwa kushika chati ghafla katika anga za muziki wa Kenya.

Nyimbo zake zimeanza kuonekana kwenye vituo vya Televisheni vya Channel O na MTV Base. Katika kipindi kifupi, kipaji cha muziki cha Jay A kimewadatisha baadhi ya wanamuziki wakongwe nchini Kenya, ambao walimpa mchongo wa  kushiriki katika nyimbo zao  kama vile STL, mwimbaji wa kike anayeishi Norway ambaye amepata umaarufu kote barani Ulaya. 

Jay A amesharekodi zaidi ya singles 12 na hadi sasa pakua video saba ambazo zimekuwa gumzo.  Wimbo wake mpya wa ‘Dumbala’ kwa sasa umeshika chati na kupigwa kwenye vituo vingi maarufu vya redio na televisheni nchini Kenya.  Nyimbo zote ambazo ameshirikishwa, zimekuwa zikishika chati na kupata umaarufu mkubwa, mmojawapo ni “Ligi Soo” ambao umewashirikisha wasanii maarufu 10 wa Kenya na yeye alipewa  heshima ya kuimba sehemu ya mwanzo ya wimbo huo, na tokea  kipindi hicho wimbo huo umekuwa kukitafutwa kwenye mitandao ya intaneti  nchini  Kenya. Jay A alishiriki pia kwenye single ya ‘Do Nurff’, ‘Doing it Right’, na single ya STL ‘Stella Stella Stella’   na kwenye Remix ya Octopizo, ‘Bill Mike. Yeye mi mtunzi wa nyimbo zake zote ambazo zina ladha za hip-hop, Rnb na aina nyingine.

Alianza kuimba akiwa na umri mdogo na alikuwa  bado  yuko  shule ya msingi. Jay A njozi maalum; yeye alidhamiria kutengeneza muziki mzuri ambao kila mmoja ataukubali.  Anahisi kuwa sehemu kubwa zaidi ya fans wake ni teenagers. Ratiba yake kabla ya kwenda kwenye jukwaa ni kusali (Jay A ni Muislamu).  Hupendelea ku-chill na best wake mkubwa Ali, ambaye pia ni meneja wake. Jay anasema kitu alichojaaliwa chenye thamani kuliko vyote ni sauti yake.