JACKIE CHANDIRU

NCHI ALIYOTOKEA: UGANDA
AINA YA MUZIKI: RNB

 

KURASA ZA KIJAMII

   

Jackie ni mmoja wa wasanii na wanamuziki wanaotamba na muziki wa Rnb Uganda.  Alianza kazi ya muziki mwaka 2004 baada ya kuibuka kuwa mmoja wa washindi wa Coca Cola Pop Star.  Ushindi huu ulikuwa ni sehemu ya chachu ya  kuundwa kwa kundi la Blu 3, ambalo lilikuja kuwa kundi la wanawake linalotamba barani Afrika. Mnamo mwaka 2010 Blue walipumzika, hivyo kuwafanya wasichana hawa kufanya kazi kwenye miradi yao wenyewe.  Katika mwaka wa 2010, Jackie alitoa rekodi yake ya kwanza iliyoitwa “Agassi” kwa lugha ya Lugbara (lugha yao ya kienyeji) na lugha ya Kiingereza.  Wimbo huu, ulimpatia hadhi ya kuwa msanii bora wa kuijitegemea na ulimpatia tuzo ya mwimbaji bora wa Rnb kwenye tunzo za Diva zilizopita.

Jackie ni miongoni mwa wanamuziki wachache wa Uganda waliofanikiwa kuvunja mipaka ya nchi yake na kuingia katika anga za Afrika nzima.  Yeye anasema, “Style ya muziki ni vigumu sana kuuiga  kwa sababu ninafanya kwa ubora zaidi kila kitu ukitoa vionjo vya Jazz hehe…  ni mchanganyiko unaoleta ladha maalum ya Jackie” Sehemu kubwa ya nyimbo zake huwa anaziandika mwenyewe, na chache zilizobakia huwashirikisha waandishi wenzake.  Matamanio yake ni kuridhisha moyo pamoja na kukataa kushindwa.  Angependa kukumbukwa kwa minenguo yake na jinsi anavyomudu kukonga mioyo ya washabiki, kiasi ambacho watu hawakutarajia kutoka kwa mwanamke. Anasema,  changamoto ni sehemu ya maisha yake.

KURASA ZA KIJAMII