IYANYA

NCHI ALIYOTOKEA: NIGERIAN
AINA YA MUZIKI: AFRO POP, RNB

 

KURASA ZA KIJAMII

   

Iyanya  Mbuk alianzia kuimba  kwenye  kwaya kanisani  kwao  na  alikuwa  mwalimu kiongozi  wa  kwaya ya watoto  akiwa  na  umri  wa  miaka  5 tu. Baada  ya  kumaliza  masomo katika Chuo  Kikuu  cha  Calabar  alipata  Shahada  ya  Uongozi  katika  Biashara, alifanya  kazi  katika  hoteli  na  aliimba nyimbo za karaoke kwenye bar ambayo yeye alikuwa meneja.  Alishawishika  kujiingiza kwenye  muziki  kitaaluma baada ya kuvutiwa na maisha ya fanaka za akina 2face,  Idibia na  Olu  Maintain. 

Mwaka  2008 kundi la  KC  Presh  lilimshawishi  Iyanya  kushiriki  kwenye shindano la kwanza la uimbaji la MTN Project Fame, Iyanya aliibuka mshindi wa kwanza na huu ulikuwa  mwanzo wa maisha ya kuziki ya Iyanya. 

Baada ya kushinda MTN’s Project Fame, Iyanya alianza kurekodi albamu yake ya ‘My Story.’  Albamu hii ilishindikana kumpatia faida yoyote kutokana na mapungufu ya usambazaji na  promosheni.

Baada ya kutembelea mji alikozaliwa wa Calabar na kuona watu wamevutiwa na dansi ya Etighi, Iyanya aliamua kufanya muziki utakaoutangaza uchezaji wa tamaduni ya Calabar.  Alishirikiana na mtayarishaji muziki DTunes na kurekodi single ya ‘’Kukere” ambayo  ilikuwa  na  mafanikio makubwa  duniani, hususan  Nigeria, Ghana na  Uingereza. Wimbo huo  ulifuatiwa  na  single yake ya pili  iliojulikana  kama  ‘’Ur waist’’.