DIAMOND PLATNUMZ

NCHI ALIYOTOKEA: TANZANIA
 AINA YA MUZIKI: BONGO FLAVA, AFRO POP

KURASA ZA KIJAMII

   

 

Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond Platinumz (au Diomond) alianza rasmi safari yake ya muziki mwaka 2006, ingawaje hadi kufikia hapo alipo ilikuwa na changamoto nyingi.  Alilelewa na Mama na Bibi yake ambao hawakuwa na kipato kikubwa.  Alionyesha mapenzi makubwa kwenye muziki tangu akiwa na umri mdogo, kipaji chake kikiendekea kukua kwa kuiga wasanii wa ndani na nje akiimba nyimbo zao kwenye matukio mbalimbali.

Baada ya kumaliza Kidato cha Nne mwaka 2006, Diamond alijikita kwenye muziki.  Diamond alipokuwa akijitahidi kujiongezea kipato kwa kuingia studio mwaka 2007, alilazimika kujiingiza kwenye ujasiriamali, kama machinga, kuajiriwa kwenye vituo vya petroli, kuwa mpiga picha wa kujitegemea na kazi nyingine yoyote ambayo aliona itamwongezea kipato.  Alifikia hatua ya kuuza vidani vya dhahabu vya mama yake kwa siri ili kuweza kulipia gharama za studio.  Hatimaye alirekodi wimbo wake wa kwanza ambao haukubamba kwenye chati sana lakini ulimfungulia mlango na kumuanzishia  rasmi safari yake kama msanii wa Bongo Fleva.

Kupitia wimbo wake huo Diamond alikutana na Chizo Mapene ambaye alijitolea kuwa Meneja wake. Makubaliano yao yalikuwa ni kutengeneza albumu, lakini bahati mbaya waliishiwa fedha na hivyo uhusiano wao kikazi uliisha bila pakua album hiyo.  Hivyo Diomond alinyong’onyea sana.  Ndoto zake ziliyeyuka na kiu yake ilitiwa majaribuni; uhusiano na ulisitishwa na marafiki waligeuka kuwa wageni.

Mambo yalianza kumnyookea Diamind mwaka 2009 pale alipokutana na Msafiri Peter a.k.a Papaa Misifa ambaye alikubali kumpa msaada wa kifedha ili kukuza kipaji cha Diamond, kibao chao cha kwanza walichorekodi kiliitwa “Nenda Kamwambie”, ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya mpenzi wake ambaye alimwacha pale alipokuwa hana kitu.  Huo ndicho kibao kilichofungua milango kwa Diomond katika ulimwengu wa muziki.

Alivuma zaidi kwa wimbo wake uiliowika unaoitwa “Number One”.  Alifanya onyesho siku ya mchujo wa kuwatoa baadhi ya washiriki kwenye Jumba la Big Brother 7, mwaka 2012.  Diamond ni mwanamuziki anayependwa sana na washabiki wake na inasemekana kwa sasa ndiye mwanamuziki anayependwa na kuandikwa zaidi Tanzania, kwenye tasnia ya muziki.  Inaaminika kuwa ndiye msanii aliyeuza sana miito ya simu kwenye makampuni ya simu mwaka 2013, ikiwa ni pamoja na kuwa miongoni mwa wasanii wanaoingiza kipato kikubwa kwenye tasnia ya muziki wa ukanda wa Maziwa Makuu.