CHIDINMA

NCHI ALIYOTOKEA: NIGERIAN
AINA YA MUZIKI: AFROPOP

 

KURASA ZA KIJAMII

   

Muziki wa Nigeria una ushindani mkali lakini mwanadada huyu kadhamiria kushikilia nafasi yake. Safari yake ya muziki ilianza mara tu baada ya kushinda shindano la muziki. Kwa Chidimna ni msanii wa kujitegemea na pole pole kaweza kufanikiwa kuwa mmoja kati ya wasanii wakubwa barani. Uko tayari kumkaribisha sebuleni kwako kupitia Coke Studio Africa?

SAFARI YAKE YA MUZIKI

Chidinma Ekile anaefahamika kwa jina lake la kwanza au kama Ms. Kedike kutokana na ngoma yake maarufu “Kedike”. Bi’dada huyu ni mwanamuziki wa Afro-Pop kutoka Nigeria.

Chidinma alitekelezea kwenye taa za jukwaa mara ya kwanza aliposhiriki na kushinda msimu wa tatu wa MTN Project Fame Afrika Mashariki mwaka 2010

Baada ya kushinda Project Fame, Chidinma hakupoteza muda na moja kwa moja akaanza kuachia single moja baada ya nyingine na albamu ndani ya mwaka mmoja. Aliachia single yake ya kwanza “Jankoliko” aliyomshirikisha Sound Sultan mwaka 2011. Ambayo ilifwatiwa na “Kedike” mwezi wa Oktoba mwaka huohuo. Single hizi zote zilikuwa kwenye album yake ya kwanza iliyoitwa “Chidinma” ambayo iliachiwa mwisho wa mwaka huo wa 2011.

Single yake “Kedike” ilipikuwa ikipigwa kila mahali ndani nan je ya Afrika. Neno“Kedike” linamaanisha mapigo ya moyo

Ndani ya wakati mfupi, safari ya Chidinma ya muziki ilianza kukolea. Kwa msanii chipukizi, mwanadada huu kajitahidi kweli kweli. Alifanikiwa kushinda tuzo ya Best Female West African Act katika Tuzo za Kora mwaka 2012, ikiwemo na kutajwa katika kugombania tuzo nyingine pia.

WANAOMHAMASISHA KIMUZIKI

Chidinma anahamasishwa na Michael Jackson, Bob Marley, Alicia Keys, whitney Houston, Maraiah Carey, Fela Kuti, Omawumi, Onyeka Onwemu, Lagbaja na Darey Art Alade

BACKGROUND YAKE

Chidinma alizifuata ndoto zake kwa kushiriki na kushinda Project Fame, iliyokuwa na washiriki zaidi ya 8000. Hii ilikuwa mwaka 2010.

Alipokuwa katika mashindano alipata mafunzo ya sauti, kucheza na mengine mengi.

MENGINE KUHUSU MS. KEDIKE

Mashabiki wake waliongezeka baada ya kusingiziwa na skendo ya kuwa alishiriki kwenye picha za utupu.


DISCOGRAPHY : ALBUM

  Chidinma (2011)