BURNA BOY

NCHI ALIYOTOKEA: NIGERIAN
  AINA YA MUZIKI: AFROFUSION

 

KURASA ZA KIJAMII

   

Burna Boy ambaye jina lake la kuzaliwa ni Damini Ogulu alikuwa akisomea tasinia ya Habari, Mawasiliano na Utamaduni, kabla ya kuacha na kujiunga na tasnia ya muziki mwaka 2010.  Kwa mara ya kwanza alitoa rekodi mbili mchanganyiko ambazo yeye anaona kuwa ni bora kuliko kuwa na albamu.  Muimbaji huyu mwenye umri wa miaka 23 alijikita rasmi kwenye tasinia ya muziki pale alipotoa rekodi yake ya kwanza inayoitwa “Freedom Style” mwezi Octoba mwaka 2010 ambayo ilimfanya ajumuishwe kwenye rekodi za Aristokrat.

Katikati ya mwaka 2011, Burna Boy alitoa rekodi nyingine yenye nyimbo mchanganyiko 13 ijulikanayo kama “Burn Notice”, ikijumuisha wimbo wa “Wombolombo Somtin”, wenye vionjo vya Angelique Kidjo, Novemba 2011 alitoa albamu nyingine “Burn Identity” yenye vibao 13 mchanganyiko ambayo ilijumuisha mtindo wake mwenyewe unaojulikana kama “Mavado’s Starboy” na nyimbo nyingine zenye mtindo wa dancehall, vibao umaarufu kama vile “Summer Time” na Ice Cream Man vimeshikilia ubora wa hali ya juu.

Juni, mwaka 2012 alitoa kibao chake cha taratibu kilichooitwa Summer Jam, kilichompandisha chati kwenye vyombo vya habari, na kumfanya atambe kimuziki kutoka Port Hacourt hadi Lagos.

Aliendeleza umaarufu kwa midundo ya Kiafrika katika rekodi zake kama vile “Tonight, Run My Race”, and Yawa Dey. Mwezi Agosti, 2013 alitoa albamu ya L.I.F.E iliyokuwa na vibao 19.

Vilevile, alishirikishwa kwenye nyimbo za Sarkodie na AKA (Special One) pamoja na wasanii wengine wengi maarufu.  Burn Boy alifunika anga za muziki kwa ujuzi wa hali ya juu na sauti ya kipekee. Amekwishafanya maonyesho mbalimbali makubwa, barani Afrika na kwenye anga za kimataifa.


LISTI YA MIZIKI : ALBAMU

Burn Notice (2011)