Who’s that, Who’s that, Who’s that?” – It’s Boity!

Mistari ya ukweli, flow kali yenye mzuka wa kigumu ila bado ina utamu; Huyo ndo Boity! Hivi karibuni ameachia ngoma inaitwa “Wuz Dat” akimshirikisha rapa mkali wa Afrika Nasty C. Tangu “Coke Studio Africa 2017”, ndo ilikuwa mara yake ya mwisho, na Coke Studio Africa 2019 anatokelezea kwenye shoo ya TV . Atakiwasha jukwaani na Nazizi (Kenya) na Lioness wa (Namibia).
 

Wuz Dat” at Coke Studio?

Miezi kadhaa baada ya kuachia wimbo wake wa kwanza, Boity aliitwa Coke Studio kuiwakilisha South Africa kwenye shoo. Boity analezea alichokiona Coke Studio kuwa “Cha kipekee” na “kimebadilisha maisha”, ameongezea pia; “Itakuwa ni kitu kitakachokuza nafasi yangu kwenye tasnia ya muziku wa rap” Wasanii wengi waliokuwa kwenye Coke Studio Africa wamepata kitu kutoka kwenye jukwaa hili, ukiacha hilo wamefanya shoo iendelee kusonga zaidi. Boity ameyasema haya kuhusu kwanini ni shoo muhimu kwake: "Coke Studio ni sawa ile nafasi nadra unayoipata ambayo unatakiwa uichangamkie na ujue nini unachohitaji ili kufikia malengo”Imenifunza kuwa naweza na nafikiri nitajaribu kutumia nguvu hii kufanya mengi”
 

A rapper at heart

Umahiri wa Boity kwenye ngoma, ni wazi kwamba mara zote amekuwa macho wazi kwenye kudondosha mistari na alikuwa anasubiri tu muda muafaka. Anaeleza: “Nilikuwa najua kuwa naweza kuchana, ni moja kati ya vitu nilivyokuwa napenda na nina furaha hatimaye nimeweza kuonesha nachoweza kwa mashabiki wangu. Ladha ya muziki wa Boity umetokana na kuvutiwa na muziki wa Kanye West, Drake, Cardi B na AKA. Baadae alipata nafasi ya kushea jukwaa moja na Migos kwenye shoo yao South Africa mwaka 2017.

Boity’s style and approach

Boity anakubalika kama mmoja wa wakali wa kwenye media waliongia kwenye uwanamitindo na uigizaji wanaopendwa South Afrika. Watu wengi walihoji na kutia shaka juu ya uwezo wake lakini Boity harudi nyuma kwenye muziki.. Anathibitisha: “Sijawahi kuwa na ujasiri kama nilionao kwenye tasnia ya muziki. Nahisi hii ndo sehemu ambayo inanifanya nijielezee. [Nina hakika kunakuwa na mengi ya kujifunza miaka ijayo].”

Kuhusu utengenezaji muziki, Boity anaelezea: “Nachohitaji kufanya ni kuwa karibu na muziki na kuacha mdundo uongee namimi, kuruhusu ubunifu wangu wote kutambaa, sio rahisi kama inavyoonekana”

Usikose kuomuona Boity kwenye Coke Studio Africa 2019 ya mwisho, akiwa na wakali wengine wa kike wa Afrika. Sehemu zote pia zinaweza kuonekana kupitia YouTube.com/CokeStudioAfrica