TOLEO KWA WAANDISHI WA HABARI:

COKE STUDIO AFRICA INAONESHA UWEZO WA MWANAMKE KUPITIA BENDI YA COKE STUDIO AFRIKA 2019

Katika kusheherekea ya siku ya wanawake duniani, Coke Studio Africa msimu wa 2019 ilitangaza sehemu yake maalumu ya wanawake wote chipukizi kwa mtindo wa kipekee ikionesha wanawake mahiri wapiga vyombo vya muziki ambao watakuwa sehemu ya bendi katika sehemu ya mwisho ya Coke Studio Afrika 2019.

Wanawake hao wanajumuisha Kasiva Mutua (Percussion), Wendy Kemunto (Muimbaji), Ivy Alexander (Gita), Naomi Ziro (Besi Gitaa) na Mutindi Tindi Muasa (Kibodi). Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Coke Studio Afrika ikishirikisha bendi yenye wanawake tupu pamoja na wapiga vyombo vya muziki wanawake katika hatua madhubuti iliyolenga kumulika vipaji mahiri kutoka afrika na kuwapa nafasi wanawake katika Sanaa.

Mshiriki wa TEDGlobal 2017, Kasiva Mutua mwaka huu anafanikisha kwa mara ya pili kuingia kwenye Coke Studio Africa na anasema haya kuhusu alichopitia. “Imekuwa ni hamasa kweli kweli kufanya kazi na wasanii mbalimbali kutoka Afrika na kufurahia utu wao kitu ambacho kinanijenga ninapotengeneza muziki. Kama mpenzi wa wa vyombo vya asili vya muziki ninakubaliana na suala kwamba katika msimu huu, Coke Studio Afrika imeweka vitu vingi vya namna hii”.

Kuwa ametumbuiza katika majukwaa tofauti tofauti ndani na nje ya nchi, Kasiva anaielezea Coke Studio Africa kama gurudumu la yeye kujifunza “ Coke Studio siku zote imekuwa ikinipa changamoto za kunijenga, unatakiwa uchimbe kwa kina, ufanye uchunguzi na uzungumze na wasanii ili kupata mawazo yao.

Miaka michache iliyopita nyota wa Kenya anaechipukia, Kemunto aliweka chapisho la nguvu, toleo la Kiswahili la wimbo wa msanii Yemi Alade na Sauti Sol unaoitwa “Africa” katika kurasa zake za mitandao ya kijamii na malikia huyo wa Afrobeat (Yemi Alade) afrika akarudia chapisho hilo pia. Hii ilikamata macho na masikio ya waandaaji Coke Studio Africa ambapo waliamua kumpa Wendy nafasi kama muimbaji wa sauti ya nyuma wa Coke Studio. Sasa muimbaji huyu anaepeperusha bendera kama muimbaji na mwandishi wa muziki hawi kama tu msaidizi wa kuingiza sauti wa Coke Studio ispokuwa akisimama kama msanii mwenyewe pembeni akiwa na mtayarishaji muziki kutoka Kenya Joe Mutoria ambae ameshiriki kutengeneza Nyimbo ya Coke Studio Africa 2019 #MadeInKenya. Kemunto amefunguka kuhusu kolabo yao inayokuja: “kupewa nafasi ya kufanya wimbo katika jukwaa kubwa kama lile ina maana kubwa sana kwangu”, Kemunto aliongeza kwa kusema, “Mara ya mwisho nilikuwa msaidizi wa muimbaji na sasa imekuwa tofauti kuingia Coke Studio Africa kama msanii! Inasisimua kidogo lakini inaleta furaha.

Kutoka kufanya maonesho mbalimbali katika majukwaa makubwa kama vile safaricom International Jazz Festival, mpiga gita Ivy Alexander anajiunga na Coke Studio Africa kama mpiga gita wa kwanza wa kike wa Coke Studio. Akizungumzia alisema : ” Uwepo wangu Coke Studio ni wa kushangaza na kufurahisha kwa sababu nimepata nafasi ya kukutana na wasanii ambao sikuwahi kuwaza ningekuja kukaa nao pamoja, kitu ambacho kinanifanya nikiri kwamba kimenifanya nikue kimuziki. Kupitia Coke Studio nimekutana na watayarishaji wa muziki na wasanii ambao natumai nitafanya nao kazi nje na Coke Studio Afrika.

Ivy anaendelea kutilia mkazo nafasi yake kimuziki wakati huo huo akitengeneza kazi zake

Binafsi

Kutoka kunoa ujuzi wake kama mpiga kibodi, mpiga besi na muimbaji, Tindi ametumbuiza na Bendi ya Gravitti, Flower Project na June Gachui. Hii ni mara yake ya kwanza kwenye Coke Studio ambapo anakiri kwamba ilikuwa mshtuko kwake: “ Kila mmoja angependa kushiriki kwenye Coke Studio Afrika lakini sikuwaza kama ingekuwa haraka namna hii. Uzoefu umekuwa wa muda mfupi na wa kushangaza. Kujifunza lugha tofauti tofauti na kuelewa mitindo ya muziki inaumiza kichwa kidogo. Coke Studio ni jukwaa la ndoto yangu, kwahiyo siwezi kuichukulia hiyo rahisi rahisi. Ni Baraka

Angalia msimu mpya wa Coke Studio Afrika kila Jumapili saa 2 kamili usiku kupitia Citizen TV, KISS TV, K24 TV ST Swahili; Saa 4 kamili usiku kupitia KTN na NTV na Saa 10 kamili jioni kupitia Switch TV Kenya. Shoo hii pia huruka kila Jumatatu saa 5 kamili asubuhi kupitia Maisha Magic East. Kupitia redio Coke Studio huruka kila jumamosi saa 8 mchana kupitia Redio Citizen, Redio Maisha, Milele FM, Nation FM na redio NRG.

 

DOKEZO LA WAHARIRI

Coke Studio Afrika ni onesho la muziki lisilo la ushindani ambalo hulenga kuwaleta wasanii pamoja na kufurahia vipaji mbalimbali vya muziki wa kiafrika. Pia huwapa nafasi wasanii chipukizi kufanya kazi na wasanii wakubwa wa nyumbani na hata nje ya mipaka ya nchi zao ikiwa pamoja na vipaji katika uzalishaji wa muziki.

Wasanii wa aina mbalimbali huchukuliwa kutoka maeneo tofauti na huwekwa pamoja ili kutengeneza muziki halisi na wa kisasa wenye mahadhi ya kiafrika. Wasanii hushirikiana na kuzalisha muziki kwa msaada wa watayarishaji wa muziki huku wakipata nafasi ya kujifunza muziki na mitindo ya kila mmoja wao wakati huo huo wakipata nafasi ya kubadilishana tamaduni zao. Coke Studio huchukua watazamaji ndani ya studio ya kurekodia muziki ili kuangalia aina mbalimbali za wasanii. Wadau wakuu wa Coke Studio Afrika mwaka 2019 ni: Sankara Hotel, PACE Africa, Yallo and Home 254.

 

Tupate:

YouTube: www.youtube.com/cokestudioAfrica

Facebook: www.facebook.com/cocacola

Blog: www.cokestudioafrica.com

Instagram: @CokeStudioAfrica

Twitter: @CocaColaAfrica

Hashtag: #CokeStudioAfrica