Kujiweka sawa: Weasel amerudi Coke Studio

 

Weasel ni moja kati ya watumbuizaji wanaoheshimika zaidi Afrika, akijulikana zaidi kutoka katika kundi la muziki linalofanya vizuri zaidi Uganda – Radio & Weasel. Tangu kutokea kwa kifo cha Radio, Weasel amelazimika kuwa msanii wa kujitegemea. Radio & Weasel walifanikiwa kuingia kwenye Coke Studio kwa mara ya kwanza mwaka 2016. Mwaka 2019 Weasel anarudi tena kwenye shoo ili kutoa shukrani maalumu kwa kaka yake aliyemtoka na mashujaa wengine ambao Afrika imewapoteza.

 

Kumuenzi Radio

 

Kwa ngoma kali zilizotikisa Afrika kama vile “Magnetic”, “Hellena”, “Breathe away” na “Don’t Cry” ambayo amemshirikisha Wizkid, Weasel ana muonekano mzuri katika ramani ya burudani Afrika, akipata tuzo mbalilmbali kama vile Hipipo (Uganda) na tuzo za muziki Tanzania bila kusahau kuchaguliwa kwake katika kuwania tuzo mbalimbali kama vile tuzo za BET na MTV. Kifo cha radio kilikuwa ni pigo kubwa kwa Weasel na tasnia ya burdani Afrika kwa ujumla. Hata hivyo Weasel anaendelea kupona kutokana na jeraha hilo na anaweka wazi hili: Mimi na Radio ni marafiki ambao tulikuwa kama ndugu na tulifanya kila kitu pamoja. Inaumiza sana kumpoteza mtu kama yeye lakini hakuna namna ninayoweza kufanya. Natumaini kupata neema na amani ili kusonga mbele kwa sababu bado sijakaa sawa.

 

Mipango ya kutoa Nyimbo mpya

 

Kutokana na kifo cha Radio, Weasel hajapanga kupunguza kasi katika harakati zake za muziki. Kinyume na hilo katika kupambana zaidi anategemea kutoa albamu yake mwaka huu 2019 pamoja na baadhi ya nyimbo ambazo Radio hakuzitoa enzi za uhai wake. Weasel anadhihirisha: “ Tayari nina albamu yenye Nyimbo 15 ambayo nimewashirikisha baadhi ya wasanii kama vile Chameleon, King Saha, Pallaso na Messiah. Nategemea kuiachia albamu hii 2019.

 

Kurudi kwenye Coke Studio

 

Radio & Weasel walishirikiana na kundi kutoka Togo – Toofan kwenye Coke Studio Afrika mwaka 2016 kutengeneza baadhi ya Nyimbo kama vile “Shuga Danse” ambayo ilitengeneza na mtayarishaji mahiri kutoka Kenya Madtraxx. Katika msimu wa Coke Studio Afrika mwaka 2019 Weasel anarudi tena na sasa akishirikiana na muimbaji mwenzake kutoka Uganda King Saha na Yared Negu kutoka Ethiopia katika toleo maalumu la kuwapa heshima watoa burudani kutoka Afrika. Anasema: “ Natumaini kufanya kazi Coke Studio Africa kutanisaidia kusonga mbele kama msanii wa kujitegemea na hivyo watu wataupenda muziki wangu”.