4 Things You Didn’t Know About Nadia Mukami

Mkali wa Kenya anayekuja kwa kasi Nadia Mukami amepata umaarufu kufuatia mafaniko ya ngoma yake iliyobamba ya “Yule Yule”, “African Lover” na “Si Rahisi”. Tangu 2015 amekuwa akiwashangaza mashabiki wa muziki wa Kenya kwa sauti yake yenye nguvu na mashairi ya kukaririka. Mwaka 2019 atatokelezea kwenye Big Break ya Coke Studio Africa akiwa na mwimbaji wa R&B Jux na mwimbaji wa Zambia Shellsy Baronet. Nadia anaendelea kuongeza spidi ya safari ya muziki wake.

Taarab Music

“Naweza kusema safari ya muziki wangu ilianza nilipokuwa mdogo, nikisikiliza kaseti za baba za music wa Taarab. Hata hivyo wasanii kama, Ray C na Sanaipei Tande ndio nilikuwa nikiwaangalia kwenye muziki wangu,” alisema Nadia, ambaye anasema ubunifu wake wa uandishi umetokana na mchanganyiko wa kusikiliza aina tofauti za muziki, shukrani kwa baba.

How I Got My Parents Attention

Nadia alipoanza, wazazi wake walikuwa na wasiwasi kuhusu uamuzi wake wa kuchagua muziki. Bahati nzuri, ngoma zake alizoachia kwenye media zilifanya vizuri na kumpa mafanikio ya kupata mashabiki. Hii ilifanya wazazi wake kumuelewa. Anasema “Nilipoanza, wazazi wangu hasa baba yangu, alikuwa akisita kuniruhusu kufanya muziki. Ilikuwa hadi waliponiona kwenye TV ndipo walipoamua kunipa nafasi na sasa wamekuwa watu wanaonisaidia.”

Lessons from Coke Studio Africa

Kama msanii kijana, kuna changamoto nyingi unakumbana nazo unapoanza kwenye tasnia ya muziki lakini Nadia anaendelea kujifunza kutokana na changamoto na nafasi zinajileta kwake.

“Sio rahisi kufanikiwa mapema lakini ninashukuru kwa kipindi kifupi nimekuwa kwenye ramani, milango mikubwa imefunguka. Ni miujiza niliimba kuhusu Juma Jux na Vanessa Mdee kwenye wimbo wangu wa “African Lover” na sasa Napata nafasi ya kufanya kazi na Jux kwenye Coke Studio Africa! Kipindi chote cha Coke Studio kimenifundisha kuwa ubora na nidhamu ndio kila kitu.”

If I wasn’t a musician I would be a poet or journalist

Kipindi alichokuwa Sekondari, Nadia alikuwa akiandika taarifa na kuzisoma mbele ya shule. Aliwahi kutangaza shoo iliyoitwa ‘Saturday Hip-Hop Count’ kwenye redio ya Campus Equator FM. Anasema: “Ningeweza labda kuwa mtangazaji kwenye ulimwengu mwingine.” Unaweza kuona kwenye mashairi ya Nadia kuwa yeye pia ni mshairi, hapa ndio ilipoanzia: “ Nilianza kwa kupafomu ushairi nilipokuwa Campus, hii inaonesha ushairi kwenye Nyimbo zake.”

Macho yote kwa Nadia akiwakilisha Kenya kwenye “Coke Studio Africa 2019” kwenye kipengele cha “Big Break”. Msimu uliopita wa “Coke Studio Africa 2017”, Band ya BeCa ilikuwa kwenye kipengele hiki.