Tanzania’s Latest Music Gem: Meet Mimi Mars

Alianza kutoa muziki wake mwaka 2017, mbele ya mashabiki wa muziki Tanzania, Mimi Mars, anatokea kwenye familia ya muziki, alijua kabisa kuwa atatakiwa kujituma. Miaka miwili baadae Mimi akaja na ngoma zilizotamba kama “Kodoo”, “Shuga” na “Papara” zilizopata nafasi nzuri kwenye muziki wa Bongo, mafanikio haya yamemfanya kuwepo kwenye “Coke Studio Africa 2019”.
 

Her Big Coke Studio Debut

Anawakilisha Tanzania, Mimi atakuwepo kwenye kipengele cha Big Break, kinachowatangaza wakali wengi wanaoibuka toka nchi tofauti. Anaeleza: “Kuitwa kwenye Coke Studio, na ndo kwanza nina miaka 2 kwenye muziki, inamaanisha nimekuwa nikifanya vizuri— hii ni kumbukumbu nitakayobaki nayo maishani. Ninayo shauku kubwa kuwa Coke Studio japo kuwa bado najaribu kuamini taratibu.”

Akiwa Coke Studio, Mimi atakutana na kufanya kazi na wasanii kama King Saha (Uganda) na Yared Negu (Ethiopia). Muunganiko wao wa muziki utasimamiwa na produza wa Uganda Daddy Andre.
 

Should we expect another Mdee Collabo?

Mimi Mars amesainiwa na lebo ya Mdee Music, inayomilikiwa na mmoja wa dada zake wakubwa — Mkali wa pop Afrika mashariki aliyefika jukwaa la Coke Studio Africa msimu wa mwaka 2016, Vanessa Mdee. Dada yake mwingine Nancy Hebron (zamani kama Namtero Mdee) pia ni mwimbaji wa Injili. Mimi amefuata nyayo za dada zake ambao wamemuongoza kwenye tasnia ya muziki: “Nimejifunza mengi kutoka kwa Vanessa kwa kumwangalia anachofanya na kujifunza kutokana na mafanikio na makosa yake ya nyuma. Wote yeye na Nancy wananiunga mkono.” Kipindi cha nyuma, wadada hawa watatu walishirikiana kwenye kolabo la wimbo wa “Beautiful Jesus” na Mimi amethibitisha kuwa watatu hao wameanza kufikiria kufanya wimbo mwingine.


You should maintain your originality

Ushiriki wa Mimi kwenye Coke Studio ni kutayarisha mipango ya mbeleni kuwa mmoja wa wasanii wanaotambulika barani. Anasema: “Muziki ni lugha ya kimataifa na nafikiri tunahitaji kusukuma Kiswahili zaidi Afrika. Naamini katika kuwa halisi. Ni vizuri pia kuona wasanii wengine wanaendesha muziki kwenye nchi zao. Kiukweli, nimefurahi kujifunza tamaduni tofauti. Nimechukua vitu kutoka kwa kila msanii niliyekuwa nae, na nina Imani nitavitumia kwenye muziki wangu.”


Transitioning from media to music

Mkali huyu mwenye vipaji vingi pia anatangaza vipindi vya TV na Youtube. Kutafuta uwiano sio rahisi lakini Mimi ameshangaza kwa ukuaji wa jina lake hadi kwenye hadhi ya mainstream. Anasema: “Sikuhama kutoka kazi yangu moja; nilifuata kitu nilichotaka kufanya siku zote.Kwa wakati huo, ilikuwa ni muda mzuri kufanya yote kati ya kazi nyingine na muziki, ambao ninaufurahia.

EP yake ya 2018 yenye ngoma 6: imepokelewa vizuri nyumbani.