Lioness akiwakilisha Hip Hop ya Namibia

Nyota Lioness ni rapper mkali ambaye kwa sasa anaipeperusha Hip Hop ya Namibia Afrika nzima. Kwa sasa anatamba na album yake mpya “Pride of CilQ” mabayo aliiachia mwezi Desemba mwaka 2018, amehusika kwenye episode maalum ya Coke Studio Africa 2019 – anakuwa mwana Hip Hop wa kwanza kutoka Namibia kuhusika kwenye show kali ya kushirikiana ya muziki wa Pan African.
 

Coke Studio Africa Experience

Lioness kwa mara ya kwanza atashirikiana na mkali wa kutoka Kenya anayemkubali toka kitambo Nazizi, pamoja na rapper Boity kutoka Afrika Kusini – kolabo hii imetayarishwa na mkali kutoka Kenya ambaye ni mtayarishaji pia ni mwimbaji, Viola Karuri. Ujio wa watatu hawa tunatarajia kuona tumbuizo matata lenye mseto wa muziki unaotikisa kwa sasa wenye mguso wa nguvu za mwanamke. Akizungumza kwenye show yake ya kwanza, alisema: ‘’Ilikuwa ni surprise kubwa na furaha isiyo na kifani nilipopigiwa simu. Kujiunga Coke Studio Africa ni uzoefu wa kubadilisha maisha. Sikuwahi kufikiria kabisa kama ipo siku nitakuwa hapa, tena kutokea kwenye nchi ndogo kama Namibia. Nafurahi sana kuwa kuwa sehemu ya mwanzo huu.”

“Ni mara ya kwanza kwa Hip Hop ya Namibia. Nimeheshimika kuiwakilisha nchi yangu katika jukwaa hili kubwa sababu nina mengi ya kuthibitisha kwa Afrika nzima na dunia kama tuna vipaji vikubwa nyumbani’’.
 

Safari ya Muziki

Lioness, maarufu kwa kunogesha sauti za kisasa kwenye tasnia ya muziki wa Namibia, mara kwa mara amenogesha Hip Hop ya kisasa na vitu Fulani vya michano ya zamani. Imekuwa ni msingi mkubwa wa kuachia Nyimbo kali; ambazo ‘’Dreams’’, ‘’Sauce’’ and ‘’Bad’’ akimshirikisha Slickartie. Anajivunia makubwa akiwa na project tatu kibindoni katika kipindi kifupi. Hizi ni project zake za kwanza 2015 “ILL3”, mwaka 2016 “ILL4” na album aliyoiachia hivi karibuni ya “Pride of CilQ”. Akitoa ushauri kuwapa moyo wasanii chipukizi barani, amesema: ‘’Si jambo rahisi kuwa rapper wa kike hata nyumbani, lakini kwa utashi wa bara letu tunasonga taratibu lakini tumeanza kutambulika. Unatakiwa kuwa thabiti sababu hujui lini milango yako itafunguka. Hilo ni moja kati ya funzo nililojifunza. Taratibu, ifanye kawaida na kuwa wewe nyakati zote’’.
 

Femcees mash up

Lioness amepitia mengi ya kujaribu jitihada za kufikia mafanikio ya muziki wake, na anaendelea kutengeneza, kuachia na kusambaza muziki wake mwenyewe. Anafuata nyayo za mkali wa Afro pop Freeda, ambaye alikuwepo kwenye msimu wa mwaka 2017. Akizungumzia kolabo zake kwenye msimu mpya, amesema : “Ukiwa na wakali wa michano ndani ya chumba kimoja, hakika utatarajia ushindani lakini tumeichukulia kama kolabo yetu ya kwanza. Ni wakarimu na wakali… Nimepata mitindo tofauti na ubunifu wa kipekee kutoka kwao.”