Coke Studio’s First Female Music Producer: Viola Karuri

Mwimbaji Viola Karuri, wa Kenya anayejulikana kwa wimbo “Leo” akimshirikisha Barnaba Classic na “Milele” akimshirikisha Collo, alipata umaarufu kutokana na cover ya wimbo wa kiswahili wa “Despacito” wa Louis Fonsi na Daddy Yankee, uliompatia heshima na umaarufu Afrika Mashariki.

Tangu hapo amekuwa akifanya yake kwenye tasnia ya muziki na hatimaye anaonesha upande wake wa muziki kama produza. Kwenye Coke Studio Africa 2019, Viola ametengeneza ngoma za wasnii wakike kama Boity (South Africa), Nazizi (Kenya), Keysha (Tanzania) na Lioness (Namibia) kwenye sehemu spesho inayokutanisha wanawake wakali wa Africa wanaokiki kwenye muziki.
 

A musical journey through cultures

Uamuzi wa Mhitimu wa chuo cha Berklee School of Music, kuingia kwenye muziki ulianza kwenye video ya Tshala Muana ya wimbo wa “Dezo Dezo” akiwa na miaka 8 – kumbukumbu ya wazi kwake. Alifanya kazi sana mjini New York kama injinia wa studio tofauti kabla ya kurudi Kenya, na kuzama kwenye tasnia ya muziki mwaka 2008. Alijifunza kutayarisha muziki na kuinjinia, na aliendelea hadi kuachia albamu iliyoitwa “Everything”.
 

The Ogopa-Coke connection

Ujio wake wa mwaka 2019 kwenye Coke Studio Africa unamfanya kuwa mwanamke wa kwanza produza kwenye shoo ya Coke Studio Africa. Viola anaongelea ngoma yake ya kwanza kutayarisha, anasema: “Kufanya kazi Coke Studio Africa kumesogeza muziki wangu mbele kinoma. Nimejifunza mengi kuona maproduza wengine kwenye shoo wakifanya kazi na wasanii… Imekuwa heshima kwangu kufanya kazi na wasanii ambao sikuwahi hata kufikiria ningekutana nao, achilia mbali kufanya nao.”

Kwenye shoo, Viola alipata nafasi ya kufanya kazi na mwongozaji muziki wa Coke Studio, Lucas wa record label inayofahamika sana- Ogopa DJs, na kusema: “Lucas ni kichwa cha muziki, ukikutana na utajiri wa ujuzi wake wa muziki, ni heshima kubwa kufanya kazi chini ya usimamizi wake”

Akiwa katika harakati za kusogeza muziki wake Afrika mashariki, Viola anaendelea kutoa uwezo wake kwenye tasnia kwa kutengeneza ngoma kibao.

Maproduza wengine wa Coke Studio Africa 2019 ni pamoja na produza toka Nigeria: Krizbeatz na Gospelondebeatz, Young DLC (Zimbabwe), Majic Mike (Kenya), Rophnan (Ethiopia) na Lizer (Tanzania).