Coke Studio Africa 2019 Partners

Kila msimu mpya, washirika wa Coke Studio Africa na brandi maarufu hufanya shoo hii kwenda vizuri, kwenye utayarishaji hadi hitimisho lake na kwenda hewani. Pace Africa, Sankara Hotel, Yallo Leather and Home 254— Hizi ndio brandi za makampuni ya Kenya zilizoshiriki na Coke Studio Afrika msimu wa 2019.

Keep your own Pace…

Ilianzishwa mwaka 2017, PACE Africa ni moja kati ya brand kubwa barani zinazobuni na kuzalisha vifaa vya kielekroniki vya sauti kama PACE FOCUS na PACE MATE. Pace Africa itaongeza sauti kwenye Coke Studio Africa ya mwaka 2019; Ikiwapatia wasanii na timu ya utayarishaji ya Coke Studio headphones na earphone zilizoandikwa Coke Studio. Tukizungumzia ushirika, Mkurugenzi wa PACE Africa CEO amesema: “Tunafurahi kuwepo kwenye Coke Studio Africa 2019 kwa mara ya kwanza. Tumekua pamoja kutokana na mapenzi yetu kwa muziki, ushirika huu utaletea kitu cha tofauti kwa wasanii walio kwenye shoo pamoja na mashabiki huku tukisherehekea muziki, lugha na utamaduni.”

Home away from home…

Mwaka 2019, Coke Studio Africa iliunga ushirika na moja ya brandi inayotambulika Kenya: Sankara Nairobi. Mshirika huyu wa mara ya kwanza kwenye Coke Studio ni moja ya Hoteli zenye hadhi ya nyota 5 muda wote wa kurekodi vipindi vya msimu wa Coke Studio Africa 2019. Meneja masoko wa Sankara Nairobi AJ Wangui amesema: “Kama moja ya hoteli zinazoongoza jijini Nairobi, tunafuraha kuwepo kwenye Coke Studio Africa. Sankara inatoa huduma zenye ubora na utofauti kwa wageni wetu wote. Tunafurahi kuwakaribisha wakali wetu wa Afrika msimu huu na kuwafanya wajiskie nyumbani.”

Art inspired by diverse cultures…

Yallo ni kampuni inayozalisha na kutengeneza bidhaa za ngozi zenye ubora. Msimu huu mpya, Yallo leather itatoa vitu vilivyo na jina la Coke Studio Africa kwa wasanii na mashabiki. Kuhusu ushirika mpya Mkurugenzi wa Yallo Leather amesema: “Sio kila mara kampuni ya Leather inaingia ushirika na brandi kubwa kama Coke Studio Africa, lakini tunashabihiana kimisingi, kimaono na malengo. Ninapenda jinsi wote tunaamini kwenye kutengeneza kuonesha na kusherehekea Sanaa na ubunifu wa nyumbani. Yallo, kama ilivyo Coke Studio, inajidhatiti kutoa kazi za Sanaa zenye ushawishi na zinazotokana na tamaduni tofauti.”

Kampuni hii ya leather ya Nairobi ilianzishwa mwaka 2015, na kuwa na bidhaa nyingi kama mabegi ya laptop, mabegi ya kusafiria, makasha ya ipad na tablets.

Kampuni ya mitindo ya 254 inaunda ushirika na Coke Studio Africa kwenye msimu wake wa mwaka 2019 kutoa nguo zilizo na jina la Coke Studio kwa wasanii na timu ya utayarishaji. Kampuni ni ya mavazi ya vijana ambayo imejikita kutengeneza T-shirts, Masweta, Vests na Kofia. Ilianza mwaka 2015, brandi inabeba utaifa kwenye jina lake (254 ni namba ya uwakilishi wa Kenya), na kuiweka kwenye kila bidhaa

Kujishindia mavazi na ofa kutoka kwa washirika hawa, endelea kufuatilia Coke Studio Africa kwenye mitandao ya kijamii:

YouTube: www.youtube.com/cokestudioAfrica

Facebook: www.facebook.com/cocacola

Blog: www.cokestudioafrica.com

Instagram: @CokeStudioAfrica

Twitter: @CocaColaAfrica