Masomo 5 kutoka Coke Studio Africa Master Class

Coke Studio Africa ilifanya kikao chake cha kwanza cha Masterclass katika Hoteli ya Sankara, Nairobi. Waongozaji Mugambi Nthiga na Charlie Karumi waliwaonesha baadhi ya wataalamu kutoka timu ya uandaaji vipindi vya Coke Studio Afrika. Darasa hili limetoa nafasi ya majadiliano ya kina juu ya majukumu ya kuingiliana ambayo yanasababisha mafanikio katika uandaaji vipindi, na wasemaji mbalimbali walielezea njia bora katika kuzalisha kipindi bora. Tulipata masomo tano muhimu kutoka kwenye kikao

1. Maandalizi ya kutosha ni muhimu kwa matokeo mazuri

Kazi ya mwongzaji wa sehemu za vipindi vya Coke Studio Africa, Eugene Naidoo ni kukutanisha pamoja vipande vya shoo katika mfumo wa shoo ya TV. Alisisitiza maandalizi ya kutosha kama sehemu muhimu ya uandaaji. Kwa mujibu wake: “Kujipanga mapema hufanya vitu kuwa rahisi na kuweza kuvisimamia” Kuvielewa vifaa na namna ya kuvitumia ili kukupa unachotaka ni muhimu kama vile kuchagua timu sahihi ya kusimamia bidhaa yako. Alielezea pia kuwasiliana na uongozi wa chombo cha habari ni njia sahihi linapokuja suala la utayarishaji wa kipindi.

2. Ufanisi na Ubora unahiajika kuendelea siku zote

Eugene asserted that to produce excellent content, professionals must on top of managing time and money effectively, stay consistent in whatever they do. Eugene ameeleza kuwa kuandaa maudhui mazuri, kama mtaalamu ni lazima ajali muda na matumizi ya pesa, kuendeleza ari katika anachofanya. Alisema: “Ukitaka kitu kiwe kizuri lakini kisicho gharimu, hakitokujia mapema, kama utakihitaji haraka, hakiwezi kuja bila gharama… shughuli za viwanda na za kibunifu zinatakiwa kuelewa kuwa haziwezi kufanikiwa kama hazitaelewa na kufuata wazo hili.”

3. Kufikia lengo unasapwa kuanza mapema

Muongozaji Mtendaji wa Shughuli za Kibunifu wa shoo Tim Horwood husimamia muundo na mandhari ya shoo kila mwaka. Alianza kama mwigizaji akiwa na umri mdogo kabla kuhamia nyuma ya kamera kama mpiga picha msaidizi, mwandishi wa skripti na mtayarishaji kabla ya kujiunga na MTV Base kama muongozaji pale ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza Afrika. Baadae aliendelea kukua na kuongoza kituo hiko kwa miaka kadhaa kabla hajajiunga na Coke Studio Africa. Akichangia kuhusu umuhimu wa kuwekeza kwenye tasnia ya Filamu, TV na Muziki, Tim amewahimiza wabunifu kuanza mapema “[Usione aibu kuanza] mapema Ili uongeze ujuzi. Hakikisha unajifunza zaidi kwa miaka na kujionoa ili kusogeza ujuzi wako kama unakosa heshima.

4. Kujitambua ni msingi wa kujipanga katika ujuzi wako.

Ni wazi kuwa kutambua ujuzi na uwezo wako ni hatua ya kwanza ya kujipanga juu ya kazi yako. Kupangilia mtazamo wako kutakusaidia kuwa na mengi ya kutoa na kufikisha ujumbe wako unapoanza kuingia kwenye tasnia. Tim ameelezea: “ ni sawa kuwa na hofu na uwezo na mawazo unayokuja nayo. Ni sawa kuwa tofauti au mwenye masawali mengi. Kuwa wewe na kuwa huru kama mtu, kuna mwanga ndani ya kila mmoja wetu. Kilichopangwa kuwa kitakuwa’’

5. Tumia nafasi yako kutengeneza matokeo chanya

Dunia ya leo imeungana zaidi. Taarifa na maudhui hayana gharama na hayana mipaka. Tim ameshauri wabunifu kutumia nafasi zao kutatua changamoto kwa kusambaza ufahamu, kuunganisha watu na kusaidia kutengeneza ufumbuzi kwa mabadiliko chanya Ameongezea. : “Tumia nafasi yako kusema mambo chanya. Usitoe tu maudhui ya kuburudisha. Elewa matokeo na ushawishi ulionao pale unapofanya kazi hizi. Itumie kwa manufaa ya tasnia na kuinua watu pale unapoweza.”